NGUVU ZA MIUJIZA:
Je, wajua ya kuwa kuna nguvu za asilia ambazo zipo kwa kila mwanadamu ambazo ni nguvu za ziada zenye kuitwa nguvu za miujiza?
Nguvu hizi za miujiza au nguvu za majaliwa kwa wenzetu huita psychic abilities (uwezo wa miujiza) ambazo zinategemewa kuwepo kwa kila mwanadamu katika mwili wake kutoka kwenye roho yake au kwa maneno mengine tunaweza kuita uwezo wa kiroho.
Uwezo huu wa miujiza wajinga wengi huamini ni uchawi wenye elimu na wasiokuwa na elimu wote hudondokea katika kuamini kuwa huu ni uchawi na hakuna kitu kama nguvu za miujiza pasipokuwa na msaada wa shetani.
Hapo wenye elimu za dini wanakuwa teyari wameshasahau hata majaliwa ya mitume wanaowaamini waliopewa na Muumba wao na ukiwauliza zaidi kuhusu Mitume na uwezo waliopewa wanakwambia wale ni mitume na wewe ni mtumwa(Mfuasi wao) hivyo huna lolote ulilojaliwa kwa maana yao.
Na Muumba huyo huyo kakupa akili ya kuchangamanua mambo kama haya yanapokufika maana yake kama wale ni mitume na wewe ni Mtumwa.
Huna chochote unachotakiwa kupata kama wao!
Huu ni mtizamo wa viongozi wa dini ambao elimu zao bado ndogo lakini kwa wenye elimu pana watakwambia mitume ni viongozi na waalimu wema hivyo jifunze kutoka kwao na elimu zao ni funguo za kufikia nguvu ya kiroho ambayo umejaliwa na aliyekuumba.
Hivyo unapozungumzia nguvu za miujiza kila mtu huwa nazo na anauweza wa kufikia yoyote kwenye aina hizo za nguvu za miujiza,
Nitakuorodha aina ya nguvu za miujiza hapo chini na katika makala zijazo nitakuwa nazungumzia moja baada ya nyingine na jinsi ya kuiamsha au kuifungua ili uweze kuitumia
Lengo ni kuwanufaisha watu wote na sio baadhi tu ya watu kuweza kufanya na kutumia:
Nguvu za miujiza ni ule uwezo wa kufanya jambo lisilo wenzekana likawezekana jinsi unavyotaka wewe kwa kutumia roho yako ambayo huishi baada ya mwili wa nyama kufa kuifanya ikusaidie katika yale unayotaka lakini wengi hushindwa kwa kukosa maarifa yake.
Pia kwanza kabisa elewa wewe ni roho yenye mwili na sio mwili wenye roho;
Tumia mwili wako kana kwamba ni vazi la roho yako na roho yako kana kwamba ni wewe mwenyewe.
Ni ngumu kwa baadhi ya watu kuelewa lakini ni rahisi kwa watu ambao teyari wameshaamka kiroho.
Nguvu za miujiza ndio kitu pekee kitakacho badili muondoko wa maisha yako kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine,
kutoka pale ulipokuwa huna kitu na ukawa na kitu,
kutoka pale ulipokuwa si chochote ukawa chochote
kutoka pale ambapo si mtu yeyote na ukawa mtu fulani,
Nguvu hizi za miujiza zitakufanya leo na wewe kuonekana na kusikika na kufika pale ambapo hukujifikiria kufika.
Nguvu za miujiza hujulikana pia kama mlango wa sita wa fahamu yaani kuna milango mitano ya fahamu tunayoijua ambayo ni:
- kuonja,
- kuskia,
- kuhisi,
- kuona,
- kunusa
lakini huu wa sita huwa ni hisia ambayo inakusababisha kutambua na kuamuru hayo kwa kutumia roho yako,
Milango ya fahamu mitano sote tunaifahamu na hapa tutaongelea mlango wa sita ambayo wengi huiskia tu na wengine hawajui kabisa,
kuna aina tofauti tofauti za nguvu za miujiza ambazo mtu huwa nazo au huweza kufikia moja kati ya aina hizo za nguvu za miujiza:
Ifuatayo ni orodha ya aina hizo za nguvu za kufanya miujiza huenda ukawa unazo na unafahamu au ulishawahi kufikia moja kati ya nguvu hizo za miujiza au unaweza kuanza kutambua leo
1: Apportion
(kitendo cha kupoteza kitu na kutokezesha upande mwingine)
hii ni aina ya nguvu ya miujiza ambayo mtu anaweza kuwa nayo yoyote yule bila ya kutengemea chochote au kiumbe chochote ili kuweza kufanya hili kutokea. Mfano unapoteza shilingi hata inatokea sehemu nyingine kwa msaada wa roho yako mwenyewe.
2: Astral Projection
(uwezo wa kutenganisha mwili na roho/kutoka nje ya mwili) hii ni aina ya nguvu ambayo mtu yeyote anaweza akawa na uwezo wa kutoka nje ya mwili endapo akitaka kutoka nje ya mwili wake na kufanya anachotaka kufanya katika ulimwengu wa kiroho kama kusoma,kusafiri n.k
3: Aura reading
(kitendo cha kutazama na kusoma mvuke unaozunguka kiumbe hai)
mvuke huu huweza kuonyesha yale mtu unayotaka kujua kutoka kwa mtu lakini pia Aura ni Kiwingu cha roho inayomzunguka kiumbe hai au kiumbe chochote.
4: Automatic writing
(kitendo cha mtu kuandika kitu chenye maana kubwa bila kujua na kutoa maelezo ya kina ya jambo fulani kwa kuandika)
Bila kujua ujumbe unakuwa unatoka kwenye roho yako.
5: Clairaudience
Uwezo wa kupata habari kutoka umbali usiokua wa kawaida huenda ukasikia sauti za viumbe kichwani kwako au ukasikia watu wanaongea mtaa wa pili kwa sauti za kawaida na ukienda kuuliza wanasema ndio walikuwa wanaongea hicho.
6: Claircognizance
Uwezo wa kupata ujuzi wa akili kwa njia ya ujuzi wa ndani yako au akili yako mwenyewe inakuwa inakufundisha vitu bila kusoma kwa mtu au kufundishwa na mtu unakuwa unajua na kutambua mambo bila kufundishwa.
7: Clairgustance/Psychic Taste
Uwezo wa kutambua kiini cha maelezo ya kitu kwa kuonja au kutambua hali ya mtu akiwa karibu na wewe kuhisi ladha ya kitu alichokula ukimfikiria bila ya yeye kusema unakuwa umejua
8: Clairolfactance
Uwezo wa kupata habari za kiroho au nafsi kupitia harufu yaani unaweza hata kunusa harufu ya mtu mwenye roho mbaya kupitia harufu ya kiroho au maradhi ya kiroho.
9: Clairsentience
Uwezo wa kutabiri na kupata uchambuzi wa kitu kwa kuhisi/kukisia.
10:Clairvoyance
Uwezo wa kutambua mtu, kitu, mahali, na matukio ya kimwili kupitia mtazamo wa ziada.
11: Divination
Uwezo wa kupiga ramli kwa kutumia vitu fulani fulani kama karata,namba,herufi,shikeli,simbi n,k,
12: Dowsing
Uwezo wa kufuatilia kitukilichojificha kwa kutumia kifaa ndugu kama vile kutafuta kitabu kwa kutumia karatasi ikawa inakuvuta kilipo pale tu utakapo kishika au kutafuta mali chini ya adhi kwa kushika mali nyingine au kupima maji kwa kutumia nazi mkononi yaliyopo chini ya ardhi
13: Energy medicine
uwezo wa kuponya mtu kupitia roho yako mwenyewe au imani uliyo nayo nguvu ya uponyaji.
14: Hydrokinesis
Uwezo wa kuongoza maji unavyotaka kama vile kuchezesha maji kwenye chombo bila kugusa
15: Levitation or transvection
Uwezo wa mtu kupaisha au kuinua mwili wake kwenda juu bila msaada wa chochote
16: Mediumship or channeling
Uwezo wa kuzungumza na roho zingine kama (majini,malaika,wafu,wanyama,wadudu).
17: Precognition or premonition
Uwezo wa kuona jambo lijalo baadae kwa kupitia ndoto au kwa kupitia mgando wa akili yako kama ukiwa umezubaa au unaskiliza jambo usiloliona.
18: Prophecy
Ni nguvu ya unabii wa kusema kitu kinachotokea wakati uliopo,uliopita na ujao pia muda fulani tofauti yake na precognition,
Unabii unakuwa unajua yanayotokea kwa clear images na unaweza kujua au kutokujua lini itatokea na inategemea na ujumbe unavyopata kutoka kwa aliye kuumba(Ieleweke unabii uliishia mwisho kwa mtume wa mwisho peke yake kwa imani ya dini ya Kiislam)
Sasa precognition unakuwa unaona tukio lijalo lakini hujui ni lini hadi siku limefika ndio unakumbuka hili niliona watu hawatakuamini hadi uwe umeweka record na humu ndio hutokea manabii wa uongo wengi tu.
19: Psychic surgery
Uwezo wa kuondoa maradhi kwenye mwili wa mtu yaani upasuaji wa kiroho bila kumchana kwa mavisu na kumfanya apone kimiujiza kama uvimbe wa ndani na maradhi yanayohitaji upasuaji ni aina nyingine pia ya nguvu ya uponyaji
20: Psychokinesis or telekinesis
Uwezo wa kuamuru au kuhamisha maada kwa kutumia fikra yako yaani kusukuma na kuongoza kitu kihame kwa fikra zako mwenyewe.
21: Psychometry or psychoscopy
Uwezo wa kujua kitu au maelezo ya mtu au kitu kwa kukigusa yaani ukigusa tu kitu unajua hata kwa kupima maradhi ya mtu mikosi n.k kwa kumgusa
22: Pyrokinesis
Uwezo wa kuongoza moto jinsi utakavyo yaani unaweza kuanzisha moto au kuwasha moto kwa nguvu ya roho yako.
23:Remote viewing, telesthesia or remote sensing
Uwezo wa kuona na kujua kitu kilichopo mbali ambacho hakionekani kwa macho ya kawaida yaani uwezo wa kuona vitu vilivyo mbali sana kwa macho ya kawaida
24: Retrocognition or postcognition
Uwezo wa kuona mambo yaliyopita au matukio yaliyopita miaka ambayo hata hukuwepo,
Na historia ya vitu au watu katika ndoto na vile vile ukiwa kama umezubaa unapata maono.
25: Second sight
Uwezo wa kuona jambo lililopita au lijalo kwa mfumo wa maono uwezo wa mtu kuona habari, kwa njia ya maono, juu ya hafla za baadaye kabla ya kutokea(utambuzi) au kuhisi uwepo wa mtu au tukio dakika chache kabla halijatokea.
26: Scrying
Ni aina ya nguvu ambayo mtu huwezo kuchunguza/kuona vitu vingi kwa wakati mmoja na kupata habari kwa kutumia kitu alichoshika au kwa swali analotaka kulipatia majibu kama kusoma michoro/minyaa/pesa na kupata kitu kimoja ulichokua ukitafutia maelezo yake.
27: Telepathy
Uwezo wa kuhamisha mawazo na fikra zako kwenda kwa kichwa kingine na kuanza kukiongoza unavyotamani na vilevile uwezo wa kuchukua habari zilizojificha kwenye akili ya mtu bila yeye kujua.
28: Thoughtography
Uwezo wakuchoma picha na kupoteza vitu kwenye kichwa cha mtu na kuvisahau moja kwa moja.
Kwa kutumia kichwa chako mwenyewe unaweza kumtoa mtu fikra mbovu na kuzifuta.
Nguvu za miujiza ni nguvu ambazo ziliwekwa ili watu wazitumie katika kurahisisha mambo yao mengi ambayo yatakuwa yamewazidi na hawana jinsi.
Ili kuzitumia ziweze kuwasaidia pale wanapokwama lakini kwa bahati mbaya hali jinsi ilivyo sasa hivi nguvu hizi zimefichwa na utandawazi na kuonekana ni Hadithi za kale ambazo watu leo wanatumia kuigizia movies nzuri na kuzidi kupumbaza akili za wengi kwamba hakuna kitu kama nguvu za miujiza zaidi ya kua ni hadithi za kale na uchawi na mambo ya kufikirika,
Maana wengi wameweza kuzisikia na kuzitambua baada ya kuangalia baadhi ya Filamu nyingi na kuamini moja kwa moja ni mambo yasiyowezekana.
Sasa na wewe ndugu yangu kabla hujasema ni hadithi za kale na ni mambo ya kufikiria jifikirie kipi kinachokufanya uweze kufikiria ni mambo yanayofikirika tu na hayana ukweli wowote wala faida.
Huku ukizidi kutembea humu duniani kama mwili mtupu na hali ya kuwa una roho.
wakati wenzio wakizitumia nguvu hizi kufanikishia mambo yao.
Jitambue ili muda usizidi kukutupa mkono
https://youtu.be/4yixcwST-Yg
https://youtu.be/rdb8bQInC1Y
Rakims